Timu ya taifa ya Vijana ya Kenya ilifunga timu ya Somalia iliyochangamka mabao 4-1 katika uwanja wa Bukhungu na kudumisha rekodi yao ya kutoshindwa katika Mashindano ya CECAFA chini ya umri wa miaka 18 ya 2023 yanayoendelea Kisumu na Kakamega Nchini humo ambapo baada ya kufungwa moja ya goli kuna tukio lilijitokeza.

Tukio hilo ambalo limesamba kwa kasi katika mitandao ya kijamii ni jinsi Wakenya walivyoupokea ushindi huo ambapo Askari mmoja aliyekuwa katika majukumu yake uwanjani hapo kutoa heshima kwa kupiga Saluti kwa vijana hao, huku watu wengi hasa wakenya wakipongeza tukio hilo na wakidai ni uzalendo hivyo apandishwe cheo.

Bado haijafahamika Askari huyo ni nani ingawa wengi wameendelea kudai kuwa anastahili hata kuongezewa mshahara akiwemo George Mario aliyeandika, “We demand promotion of the officer.this is a real patriotism,” Jumah Anthony akisema “Some cops deserves promotions and salary increase” na Abisai Remmy akiandika “Happiness comes all Corners . I loved officer’s spirit.”

Katika mechi nyingine ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Jomo Kenyatta, Mamboleo katika Kaunti ya Kisumu, Rwanda iliichapa Sudan mabao 3-0 katika mechi huku Kenya wakioongoza kundi hilo gumu wakiwa na pointi tisa waliofuzu kwa nusu fainali pamoja na washindi wa pili Rwanda (pointi 6) na Somalia inashika nafasi ya tatu katika kundi hilo gumu huku majirani zao Sudan wakirejea Khartoum bila pointi.

Risasi zarindima usiku kucha jirani na Ikulu
Epuka ulaji wa Vyakula hivi iwapo hujatia chochote tumboni