Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi amemkamata Askari
polisi ambaye alikuwa anaiba umeme wa TANESCO aliojiunganishia kinyume na sheria na kuweka swichi chooni ambayo ilikuwa inatumika kuiba umeme huo na kupelekea kukwepa kulipa Bili ya Umeme.

Kenan ameeleza kuwa wakati wa kufanya upekuzi katika nyumba anayoishi askari huyo pamoja na gari yake binafsi wamemkamata na maboksi ya viroba vya konyagi ambavyo vilishapigwa marufuku na serikali.

Imedaiwa askari huyo amekuwa akivitumia viroba hivyo kwa kujaza katika chupa za konyagi na kuziuza kwa wananchi katika baa yake.

Mbali na maaboksi ya viroba, pia wamekamata kete za Bangi 20 ambazo alizihifadhi vizuri katika pochi maalumu na kuzificha katika gari yake.

Vitu vingine alivyokutwa navyo askari huyo ni pamoja na gongo lita tano ambayo aliificha katika Buti la gari yake ndogo, Vyuma vinavyotumika katika Ujenzi wa Miradi mbalimbali vikiwa vimehifadhiwa katika Banda la Bata kiasi cha ndoo mbili, na madumu ya mafuta ya diesel yaliyojaa mafuta ambayo aliyaficha katika sebule yake.

Kihongosi amemuagiza OCD wa Jiji La Arusha kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika vyombo vya Sheria ili iwe funzo kwa wengine.

Katika operesheni hiyo Kihongosi aliambatana na OCD wa jiji la Arusha, OCCID pamoja na meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha ambaye alifika na wahandisi wa TANESCO na kukata umeme uliokuwa umeunganishwa darini na swichi kuwekwa chooni kinyume na utaratibu.

Amesisitiza wananchi kuwa wazalendo katika nchi yao kwani wao kama Serikali hawatamvumilia mtu yeyote na watashughulika na yeyote bila kujali cheo wala nafasi ya mtu.

“Lazima kila mwananchi aunge mkono jitihada za serikali kwani kila mmoja anaona namn mheshiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anavyopambana kuijenga nchi hii kiuchumi hivyo lazima tumuunge mkono kwa kulinda miundombinu ya serikali,” amesema Kihongosi.

Serikali yatangaza ajira 5000 za walimu
Trump apata pigo jingine Georgia