Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amemfukuza kazi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa akisimamia kwenye kituo cha Malinyi, PC Hamisi kwa kuhusika kwenye udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka uliopita.
Askari huyo alikuwa mmoja wa maafisa usalama waliokuwa na jukumu la kusimamia mitihani hiyo katika kituo hicho, wakati mitihani ilipofanyika mwaka 2018.
Aidha, askari huyo alitajwa kuwa moja ya watu ambao walipanga njama kuhusu zoezi la ufanyaji wa mitihani katika kituo hicho, ambapo alisababisha wasimamizi wa mitihani kutilia shaka kituo hicho na kuanza kukifanyia uchunguzi.
Hata hivyo, Januari 24, 2019 Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilitangaza matokeo ya kidato cha nne ya amwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38, huku likifuta matokeo ya shule moja.