Jeshi la polisi nchini Kenya linamshikilia askari wa jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne katika kijiji cha Komomange, Kuria Magharibi, Kaunti ya Migori.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kuria, Cleti Kimaiyo amekaririwa na Citizen TV akieleza kuwa afisa huyo anayefahamika kwa jina la Harrison Joseph, ambaye alikuwa amejificha tangu Julai 24, 2020, alikamatwa Jumamosi iliyopita.

Alisema kuwa tukio hilo la kikatili lilitokea majira ya saa kumi na mbili jioni ya Julai 24, 2020 na liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Kehancha.

Kamanda Kimaiyo ameeleza kuwa mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Kehancha na aliruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupatiwa matibabu.

Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi na anatarajiwa kupandishwa mahakamani mapema leo.

Taarifa za kukamatwa kwa afisa huyo wa polisi zimeripotiwa wakati ambapo kumekuwa na kesi kadhaa za vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto katika Mkoa wa Kuria.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 24, 2020

JPM achangisha millioni 48 ujenzi wa msikiti

Video: FC Bayern Munich bingwa UEFA
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 24, 2020