Afara Suleiman – Babati.
Askari wanaoingia kazini, wametakiwa kujiepusha na matumizi ya vilevi ikiwemo Pombe kwani ni kinyume na sheria, utaratibu na kanuni za Jeshi.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Lucas Mwakatundu hii leo Oktoba 4, 2023 wakati akizungumza na Maafisa, wakaguzi na askari viwanja vya FFU Manyara.
Amesema, baadhi ya Askari wanatuhumiwa kuingia kazini wakiwa wamelewa na wengine hutumia vilevi wakiwa kazini, kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa Sheria huku akiwataka pia kuishirikisha jamii katika kuzuia na kutanzua uhalifu, kama dhana ya Polisi jamii inavyotaka.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, limeendelea kujipanga kwa matukio ya Kitaifa yatakayofanyika Mkoani humo, ikiwemo maadhimisho ya wiki ya Vijana na Kuzimwa kwa mwenge wa Uhuru 2023.