Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Hassan Banga amewaongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali, ndugu, jamaa na marafiki katika kuaga miili ya Askari wawili wa Jeshi la Polisi Mkoani humo.

Askari hao, ni EX. WP 7866 CPL Elizabia Hakimu Kizale na EX. H1027 CPL Patrick Thomas Salehe ambao walipata ajali Desemba 5, 2023 katika eneo la Soliwaya Wanging’ombe, wakati wanaelekea kazini kutekeleza majukumu yao.

Akiwasilisha salamu za rambirambi, Kamanda Banga amesema askari hao wamekutwa na umauti wakati wanatekeleza majukumu yao hivyo tuwaombee wapiganaji wenzetu lakini pia tuwaenzi kwa yale yote mazuri ambayo wameyafanya. Pia amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima.

Kwa upande upande Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Claudia Kitta akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema alipokea taarifa ya msiba wa askari hawa kwa masikitiko makubwa amesema askari hawa wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa na tabia nzuri hivyo sisi tunaosalia tuendelee kuiga mfano huo wa askari wenzetu katika utendaji wa kazi.

Ibada ya kuaga miili ya askari hao imefanyika katika viwanja vya Idara ya Maji Wanging’ombe imeongozwa na padri wa Kanisa katoliki Wanging’ombe.

pq

Mafuriko yauwa Kilosa, zaidi ya kaya 150 zasombwa na Maji
Idadi ya Waliofariki ajali ya Hiace Kagera yaongezeka