Askari wawili Jijini Mwanza wamefukuzwa kazi baada ya kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni meno mawili ya tembo yenye kilo 20.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Askari hao, H.5461 Enock wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani humo na H.4165 Robeth wa kikosi maalum wamefukuzwa kazi Agosti 27, 2018 kutokana na kosa hilo.

Amesema kuwa Askari hao walikamatwa Agosti 23, 2018 Mtaa wa Nyamhongolo wilayani Ilemela wakiwa na nyara hizo.

Aidha, amesema taarifa za awali zilionyesha kuwepo kwa watu wanaojihusisha na biashara ya meno ya tembo, kwa kushirikiana na kikosi kazi cha Taifa cha kupambana na ujangili Kanda ya Ziwa ambapo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Hata hivyo, Kamanda Shanna amewataka wote waliokuwa wakishirikiana na Askari hao kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi, kwa kuwa wakianza kuwasaka ni lazima watawapata kwa kuwa walifanikiwa kuwamakamata Askari hao.

 

FC Barcelona wamuweka rehani Paco Alcacer
Kamanda afunguka kisa cha mtawa kujirusha ghorofa ya tatu