Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba amewataka Askari wa Jeshi la Uhifadhi kufanya kazi kwa kufuata Miongozo, Kanuni na kuzingatia sheria, ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Uhifadhi.
Wakulyamba ameyasema hayo akiwa Jijini Arusha kwenye Warsha maalum iliyoandaliwa kwa Maafisa wa Jeshi la Uhifadhi chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, iklenga kukumbushana masuala mbalimbali ya uhifadhi, pamoja na haki za Binadamu.
Wakati wa warsha hiyo, pia Kamishna Wakulyamba alisisitiza nidhamu ya matumizi sahihi ya sare za Jeshi hilo na matumizi ya nguvu katika kukabiliana na uhalifu hususani kwenye matumizi ya Silaha.
Aidha, Wakulyamba pia amelitaka Jeshi hilo kuimarisha mahusiano mema na Vyombo vingine vya ulinzi na Usalama, taasisi za Serikali na wananchi kwa ujumla kuwa kazi ya uhifadhi ni jukumu la kila Mtanzania kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.