Askofu na Mwenyekiti wa kanisa la Good News For All Ministry Charle Gadi ameandaa mkutano kwa ajili ya maombi ya siku 1001 kwa taifa la Tanzania.

Askofu Gadi amesema kuwa Mkutano huo wa kuliombea Taifa unatarajiwa kufanyika siku ya jumanne ya kila wiki katika viwanja vya Biafra vilivyopo jijini Dar es salaam.

“Tumeandaa maombi mengine ya siku 1001yatakayofanyika kila jumanne ya wiki kwa kadiri Mungu atakavyotupa nafasi ambayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Biafra,” alifafanua Askofu Gadi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, katika kipindi cha siku 1001 zitatumika katika kuliombea Taifa na kuhamasisha wananchi kupitia maombi kuwa na utayari wa kulipa kodi na ushuru ili kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.

Pia kuombea na kuhamasisha wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya Taifa kama vile barabara, shule, hospitali, madaraja, reli, viwanja vya ndege, majengo ya Serikali na vyuo ili viweze kudumu na kuendelea kuhudumia wananchi.

Aidha, Askofu huyo ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwenye maombi hayo kwani maombi hayo yana manufaa makubwa kwa taifa

Baadhi ya Haya Yatakufanya Ushinde Usahili
Fid Q kuandaa Script ya Wimbo Mpya wa Bella