Askofu Mkuu wa Dayosidsi ya Dar es salaam wa Kanisa la Anglikani, Dkt Valentino Mokiwa ambaye yuko kwenye mgogoro na mkuu wake, amehudhuria misa maalumu ya kuombea amani katika Dayosisi hiyo, huku akisema kuwa Kanisa hilo limeingiliwa.
Misa hiyo imefanyika katika Usharika wa Mtakatifu Albano ulioko katikati ya Jiji la Dar es salaam chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.
Ibaada hiyo imefanyika huku kukiwa na mgogoro kati ya Dkt. Mokiwa na Askofu Mkuu wa Anglikana Dkt. Jacob Chimeledya ambaye alimtaka kiongozi huyo wa kiroho ajiuzulu kutokana na tuhuma za ubadhirifu.
“Nasema mwenye ushahidi wa chochote ajitokeze, kama mambo ya karatasi karatasi yanasumbua watu, wezi wanajulikana na mimi nawajua na ushahidi ninao,”amesema Dkt. Malasusa.
Hata hivyo wakati Ibaada ikiendelea, askari wa Jeshi la Polisi waliovalia sare walikuwa wakilinda nje ya jengo la Kanisa na wamewakamata watu wawili wote wanasadikika wanatokea Usharika wa Magomeni, na kwamba walitaka kuingia kanisani hapo na mabango kuonyesha kupingana na misa hiyo.