Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Bianadamu kwa Jamii ya Viongozi wa Dini, Askofu William Mwamalanga, amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kumtaja Freeman Mbowe kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa kamati yao ilitilia shaka Klabu ya Bilicanas iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya Mbowe Hotels, kwamba ni moja ya maeneo yanayotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kufanya biashara zao pale lakini si mwanasiasa huyo.

“Sisi tulisema Club ya Bilicanas inajihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya  kwa sababu waliingia  kwa sababu walikuwa wanaingia watu mbalimbali ambao walikuwa wakiendesha biashara hiyo, lakini hatukumtaja Mbowe kuwa ndiye anayejishughulisha na dawa hizo,”amesema Mwamalanga.

Hata hivyo ameongeza kuwa ukumbi huo wa starehe huhusishwa na biashara hiyo, lakini haimaanishi kuwa mmiliki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anahusika.

Video: Sakata la dawa lageukia majaji, Mke mume jela miaka 20
Magazeti ya Tanzania leo Februari 14, 2017