Kikosi cha Aston Villa imefufua matumaini ya kubakia Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Arsenal usiku wa kuamkia leo, na kupaa hadi nafasi ya 17.

Kabla ya mchezo huo uliopigwa Villa Park, Aston Villa ilikuwa inashika nafasi ya 18, ikiwa na alama 31, baada ya kucheza michezo 36, huku Watford iliyokuwa juu yake alikuwa na alama 34.

Baada ya ushindi dhidi ya Arsenal, klabu hiyo imefikisha alama 34 na kuishusha Watford ambayo ina alama sawa nao lakini Villa ipo juu kwa uwiano wa mabao ya kjfungwa na kufunga.

Bao la Villa lilifungwa dakika ya 27 na Mahmoud Hassan ambaye alipokea asisti kutoka kwa beki mtukutu wa Kiingereza, Tyrone Mings.

Watford ilikuwa inacheza dhidi ya Manchester City ambapo ilikubali kichapo cha mabao cha aibu cha 4-0.

Mchezo wa mwisho Villa itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya West Ham, huku Watford itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Arsenal tarehe 26, ya mwezi huu.

Villa itakuwa inaiombea mabaya Watfrod ikiwa ifungwe ama kutoa sare, huku yenyewe ishinde kwenye mchezo dhidi ya West Ham.

CRDB Marathon kurindima Agosti 16
DOREFA kusaidia usajili Dodoma FC