Mwimbaji maarufu wa miduara, AT kutoka visiwani Zanzibar amemuandikia Ali Kiba ujumbe wa wazi ambao umefichua baadhi ya mambo kati yao ambayo yalikuwa kapuni.

AT

Kupitia mtandao wa Instagram, AT ameandika ujumbe huu kwa Ali Kiba:

“My dear Brother imekua desturi ya watu kutokumbuka fadhila haya ni ya kwangu binafsi wala hayahusiani na ushabiki usiojenga heshma kwa mtu acha nikutumie barua ya wazi kwako mwaka 2006 mwishoni nilibahatika ulikua shabiki mkubwa wa wimbo wangu wa UTAONA NOMA uliniambia hayo wakati tulipokutana kwa mara ya kwanza wakati nikiwa bado mgeni wa jiji la Dar maeneo ya kariakoo mtaa wa Pemba kwa Dada Rahma Mama Swalekh na tukiishi km ndugu hapo wakati ukihit na wimbo wako wa Sinderela mtu wa kwanza kwanza kukupandisha Daladala ni Mimi #Ahsante sana kwa heshma ulionipa hata pale ilipofikia nilikuambia naacha muziki uliumua na ukaniambia upo tayari kutoa pesa mfukoni unisaidie na ukanifariji kua nitafanikiwa tu #Ahsante kwa mara ya 2 tuliishi ndugu hadi kwa wazee wetu nilifurahi zaidi kuona ushirikiano wa familia yako ktk harusi yangu misiba na matembezi sikujua hata mm siku nitakua nkombozi kwako baada ya pale kituo cha tv fulani kugoma kupiga video zako eti ya kwamba unadharau niliumia vile haupo ivyo ila show yangu ya zanzibar uzinduzi wangu ukasababisha tofauti hiyo ifutike na ukawa huru zaidi na kufanya video na mtu ambae ilikua akidhani unamaringo na hatimaye ulifanya show hiyo na ulikataa nisikulipe #Ahsante sana uliweza kuniletea Marlow studio wakati akiwa anahit mno nakufanya nae Colabo hadi leo uwowimbo haujachuja hadhi nilijua ww ni mtu wa imani baada ya Msanii fulani wakati tupo Oman mwaka 2010 alikukera sana hadi ulitaka kumpiga ila niliposimama kati huruma ikakujaa hali ya kwamba ulikosewa Ombi langu kwako Ingawa ni mipango ya #Mungu ila Unamchango mkubwa mpaka mimi kua #AT naomba kati ya Tunzo mbili nilizopata Tanzania Moja nikutunukie ww Moja iyende kwa Adam Juma Good bls you @officialalikiba @adamjuma ( kuna kitu kiba ulikua unakitafuta sana hujafanikiwa kukipata ila kwa kuthamini mchango wako ni kidogo ila kitakufurahisha sana na huenda kikakutoa mchozi nakutumia now katika Whatsup yako be happy my Bro SALUTI )(#AT na #Alikiba tumefanya jumla ya colabo 3 ya 1 #Kwanini ft #QeenDarlin ya 2 #Usikomae#nae na ya3 ni #Acha#liwachome ila 2 zimesikika moja ni nyimbo anayoipenda mama yangu hamtaisikia mnisamehe ni zawadi 4 my #Mumy

Mwalimu apigwa risasi kichwani kwa kujisaidia haja ndogo
Serikali yalitega shirika la Nyumba Nchini kuhusu 'Wabangaizaji'