Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) linatarajia kupokea ndege nyingine mpya aina ya Bombardier Dash 8 Q400 inayotarajiwa kuwasili Nchini mwishoni mwa mwezi Desemba.
Akizungumza na gazeti la Serikali la Habari Leo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa shirika la ATCL, Josephat Kagirwa, amesema kuwa ingawa hawajapata tarehe rasmi ya kuwasili kwake, lakini haitazidi mwisho wa mwezi ujao.

Kagirwa alisema hivi sasa wanasubiri taarifa ya mwisho ya kuwasili kwa ndege hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 78.

Kufikia sasa Serikali ya Awamu ya Tano imenunua ndege mpya 11, nane zimewashawasili, moja ni hiyo inayotarajiwa Desemba, mbili zinaendelea kutengenezwa nje ya nchi.

ATCL kuanza safari zake Uingereza

Kagirwa alisema ndege mbili zilizobaki aina ya Airbus A220-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 zitawasili mwakani ikiwemo moja inayotarajiwa kuwasili katikati ya mwaka na nyingine mwishoni mwa mwakani.

Miongoni mwa ndege mpya ambazo Serikali ya Awamu ya Tano ilizinunua na tayari zipo hapa nchini zikiendelea na safari mbalimbali za ndani na nje ya nchi ni pamoja na Boeing 787-8 Dreamline mbili, Airbus A220-300 mbili na Bombardier Dash 8 Q400 nne.

Simba SC yajifua Abuja, yadokezwa kuhusu Plateau United
Kocha Kaze afichua siri ya ushindi Azam Complex

Comments

comments