Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limetangaza kusitisha safari zake kwenda nchini India ambako vifo na maambukizi ya corona yanazidi kuongezeka.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Ladislaus Matindi inasema safari hizo zimesitishwa kuanzia Mei 4.

“ATCL itaondoa faini zote kutokana na mabadiliko haya, itatoa tiketi nyingine au kuwarudishia nauli zao abiria waliokuwa wamekata tiketi,” amesema Matindi.

Ili kupata ufafanuzi zaidi, Matindi amewataka abiria waliokata tiketi kupiga namba O800110045 bure.

Bocco awatahadharisha mashabiki Simba SC
Ninja: Miquissone ajipange