Soda moja inakadiriwa kuwa na vijiko 10 vya sukari ambayo ni sawa na 100% ya mahitaji yako ya sukari kwa siku, hivyo kunywa soda kila siku au mara kwa mara huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.
Wanasayansi wamethibitisha kuwa ndani ya dakika 20 baada ya kunywa soda ini linaitikia kwa haraka na kubadili sukari yote iliyomo kwenye soda na kuifanya mafuta, mafuta hayo humfanya mtu anenepe na kuwa na uzito uliopita kiasi kitu kinachoathiri afya na kuharibu muonekano mzuri wa mtu.
Pia wasayansi wameendelea kwa kuthibitisha kuwa dakika 40 mara baada ya kunywa soda, mboni za macho hutanuka, shinikizo la damu huongezeka na ini huitikia kwa kuongeza kiwango cha sukari kwenye mfumo wa mzunguko wa damu unaohusisha moyo na mishipa ya damu.
-
Makala: Vyakula vitakavyokuza nywele zako haraka na kuzipa afya
-
Serikali yalivalia njuga tatizo la nguvu za kiume
Aidha, zimeainishwa athari nyingine za soda kuwa kibofu cha mkojo kujaa na mtu kuhisi kubanwa na mkojo hivyo hujikuta kukojoa mara kwa mara ambapo mkojo huo hutoka na kiasi kikubwa cha Kalisi (Calcium), Magnesi na zinki ambazo hutumika kuimarisha mifupa.
Na masaa mawili baada ya kunywa soda hali ya kujisikia furaha/vizuri (euphoria) huisha na sukari hupungua kwenye damu na kukufanya mwenye njaa, mchovu na mwepesi wa hasira.
Hivyo inashauriwa kutumia kiasi kidogo cha soda angalau mara moja kwa wiki, tii kiu yako kwa kunywa maji safi na salama kwa ajili ya kutunza afya yako na kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari.