Mwanamke mmoja nchini Nigeria amekamatwa na polisi baada ya kujaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja akidai kuwa chanagamoto za pesa zimemsukua kufanya kitendo hiko.

Mwanamke huyo amekamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi.

Hata hivyo tabia hiyo nchini Nigeria imekithiri kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu nchini humo.

Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walipovamia “kiwanda cha watoto” katika jimbo la Imo
Miaka miwili baada ya sakata hiyo, mwanamke mwingine alishikwa alipokuwa akijaribu kumuuza mtoto wake kwa dola 90 katika jimbo la Cross River.

Nigeria ni nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu zaidi ya milioni 170 wanaishi kwenye umaskini.

Video: Mbunge mwingine aitosa Chadema
Tundu Lissu: Tusipate hofu Chadema hatujaanza kusalitiwa leo