Manchester United imeripotiwa kupigwa chini juu ya ofa yao ya pauni milioni 15 kwaajili ya kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez.

Mwandishi wa Hisania Guillem Balague amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa klabu ya Old Trafford ilikuwa mawindoni kumsaka kiungo huyo wa Kihispania.

Hata hivyo, imedaiwa Atletico kwa sasa haina mpango wa kumwachia mkali huyo mwenye umri wa miaka 21.

Louis van Gaal amekuwa kipenzi cha Niguez kwa muda mrefu ambaye uwezo wake wa kuunganisha timu na kulainisha mabeki wa timu pinzani unajulikana.

Dylan Kerr Atimuliwa Simba Sports Club
Zinedine Ziadane Ameingia Kwenye Vitabu Vya Kumbukumbu