Mzee Joe Ligon alikuwa na miaka 15 wakati alipohukumiwa kifungo cha maisha gerezani na sasa ameachiliwa akiwa na umri wa miaka 83.

Yeye ndiye mtu aliyekaa gerezani kwa miaka mingi zaidi nchini Marekani

Joe Ligon alizungumza na BBC kuhusu hali ilivyokuwa katika maisha yake ya jela.ya karibu miongo saba.

“Sijawahi kuwa pekee yangu, lakini kwa sasa ni mpweke zaidi. Ninapendelea kuwa pekee yangu kadri itakavyowezekana. Gerezani nilikuwa katika seli ya peke yangu kuanzia siku nilipofungwa hadi kuachiliwa kwangu.”

Wiki ile, akiwa na umri wa miaka 15 alishitakiwa kwa mauaji, shutuma ambayo amekuwa akiikana kila mara, ingawa amekubali katika mahojiano na mtangazaji wa runinga ya PBS kwamba aliwadunga visu watu wawili walionusurika na akaelezea kujutia kitendo hicho.

“Polisi walinipatia waraka wa kusaini ambao ulinihusisha katika mauaji. Sikumuua yeyote,”

Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kufanyika Mei 21, 2021
Sports Betting kuwa sehemu ya michezo nchini