Klabu ya Singida United, leo imetangaza orodha ya wachezaji waliowaacha katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, ambacho kilifunguliwa Novemba 15 na kitafungwa Desemba 15 mwaka huu.

Miongoni mwa wachezaji waliotemwa ni mshambuliaji Atupele Green ambaye aliwahi kuzitumikia Kagera Sugar na JKT Ruvu zote zinashiriki ligi kuu soka Tanznaia bara.

Mchezaji mwingine alietemwa na klabu hiyo ya mjini SIngida ni Pastory Athans ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Simba, huku

Mohammed Titi na Frank Zacharia wakitolewa kwa mkopo.

 

Video: Mimi sijamsaliti Zitto- Msando
Picha: Kili Stars wakijiandaa dhidi ya Zanzibar Heroes