Mkulima mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka 20 mara baada ya kukutwa na vipande vinane vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni 60.
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Jijini Dar es salaam mara baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kusema kuwa upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi sita kudhibitisha mashtaka hayo.
Aidha, Shaidi amesema kuwa kutokana na ushahidi huo Mahakama imemtia hatiani, Samwel Bwandu na kutumikia kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kukutwa na nyara hizo.
Hata hivyo, mshtakiwa ameiomba mahakama kumpunguzia kifungo hicho kwani amekaa gerezani tangu mwaka 2015, na kuongeza kuwa anania ya kukata rufaa.