Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU),  limeendelea na kuweka shinikizo kwa viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali, kuteua raia watakaoongoza nchi hiyo kama rais na waziri wake mkuu katika kipindi cha mpito.

Baraza hilo lilikutana katika mkutano kwa njia ya video jana Alhamisi, Septemba 17,  na kama ECOWAS,  Umoja wa afrika unaendelea kudai kwamba kipindi cha mpito nchini Mali kinapaswa kuongozwa na raia.

Rais wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Ismaël Chergui, amesema viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka wanapaswa kufanya uteuzi wa rais ambaye atakuwa kama rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha mpito na kuheshimu katiba ya nchi.

Aidha, AU imeungana na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS kwa kutaka kipindi cha mpito kiwe na muda wa miezi 18 bila ya mwanajeshi kuongoza nchi hiyo kama rais katika kipindi cha mpito.

Agosti 19 mwaka huu,  AU iliisimamisha Mali kwenye uanachama wa umoja huo baada tu ya mapinduzi.

IGP Sirro aongezewa muda EAPCCO
Jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wake