Afisa mmoja wa Korea kusini ameuawa kwa risasi na kuchomwa moto na vikosi vya Korea Kaskazini, wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imeeleza, ikisema ”kitendo hicho ni cha kikatili”.

Taarifa  imesema kuwa mtu huyo aliyekuwa akifanya kazi na  idara ya uvuvi, alitoweka kutoka kwenye boti ya doria karibu na mpaka na baadae alipatikana kwenye bahari upande wa  Korea Kaskazini.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini walimpiga risasi, kisha kummwagia mafuta mwili mzima na kumchoma moto, wizara imesema. Iliamini kuwa ni hatua ya kudhibiti virusi vya corona.

Mpaka kati ya pande hizo mbili za Korea una ulinzi mkali na Kaskazini inadhaniwa kuwa na sera ya ”kupiga risasi hadi kifo” kuzuia virusi vya Covid-19 kuingia nchini humo.

Tukio hilo litakuwa la pili kwa vikosi vya Korea Kaskazini kuua raia wa Korea Kusini. Mwezi Julai mwaka 2008, mtalii aliuawa na mwanajeshi katika eneo la mlima Kumgang.

Afisa huyo alikuwa kwenye doria yapata umbali wa kilomita 10 kutoka eneo la mpaka na Kaskazini, karibu na kisiwa cha Yeonpyeong, alipitoweka siku ya Jumatatu, wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imeeleza.

Afisa huyo, 45 ambaye ni baba wa watoto wawili aliacha viatu vyake kwenye boti.

maafisa wa wizara ya ulinzi Korea Kusini walieleza, wakiongeza kuwa wanaamini kuwa hii ni hatua ya kupambana na virusi vya corona.

Mauaji ya Breonna Taylor: Taharuki yatanda Marekani
Lipumba aahidi kuigeuza Kyerwa kituo cha kimataifa cha biashara

Comments

comments