Mwanamke mmoja ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kukamatwa na chui sekunde 15 tu baada ya kutoka ndani ya gari lao Beijing nchini China.

Wanawake hao wawili waliokuwa wametembelea aneo la hifadhi ya taifa walikumbwa na mkasa huo ulionaswa na kamera za ‘CCTV’. Chui huyo aliondoka na mwili wa mwanamke aliyemuua.

Uongozi wa hifadhi hiyo imeeleza kuwa watu binafsi hurusiwa kuendesha magari yao katika maeneo ya wazi ambayo wanyama wanaaminika kutokuwepo, lakini huonywa wasitoke kabisa kwenye magari yao.

Chombo cha habari cha China, Xinhua kimeeleza kuwa hifadhi hiyo imefungwa kwa muda na uchunguzi umenzishwa.

JPM Kuongoza Maadhimisho ya Mashujaa Dododma Leo
Gwajima amvimbia Makamba