Jeshi la polisi Mkoani Mara linafanya uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa mlinzi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO), David Komoko (30) kwa kupigwa risasi ndani ya Bohari ya shirika hilo mjini Musoma.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Mara, Emmanuel Kachewa amesema tukio hilo lilitokea jumapili usiku na kudai kuwa mlinzi wa kampuni ya ulizi ya jirani Security Group, Analias Katesi alipiga risasi mlinzi mwenzake na kufariki papo hapo.

Imeelezwa kuwa mlinzi huyo akiwa lindoni aliona watu wanne ndani ya uzio wa bohari kuu mmoja wao akiwa na mzigo kichwani na baada ya kuwatilia shaka, aliamua kumfyatulia risasi aliyekuwa na mzigo ambao ulikuwa na vifaa mbalimbali vya umeme.

Kachewa ameeleza kuwa baada ya Katesi kumsogelea, alibaini mtu aliyepigwa risasi ni miongoni mwa walinzi waliokuwa wakilinda bohari tena akiwa amevalia sare za kazi za shirika hilo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 26, 2019
Ulaji wa Samaki umeshuka Tanzania