Nyota wa klabu ya Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang amegoma kupangiwa namna ya kuishi huku akisisitiza kuwa, kamwe hawezi kubadili mtindo wake wa maisha eti kisa tu watu hawapendezwi nao.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Gabon amelazimika kuweka wazi hilo baada ya kuulizwa na mwandishi kuwa aina yake ya maisha ikiwemo kuendesha gari kwa kasi na kunyoa mitindo mbalimbali imekuwa ikijadiliwa sana lakini Aubameyang amesisitiza kuwa hiyo ndio furaha yake.
“Ninapenda kufanya vitu vinavyonitambulisha kuwa mimi ni nani na haijalishi kama watu wengine hawawezi kukubaliana na mimi,”amesema Aubameyang
Aidha, Aubameyang amesisitiza kuwa akiwa uwanjani anapenda kufanya vitu ambavyo vitawafurahisha mashabiki wake kama kufunga mabao mengi iwezekanvyo lakini linapokuja suala la kuishi ndoto zake za utotoni hapendi kupangiwa na mtu yeyote.
Hata hivyo, Aubameyang alitoka Borussia Dortmund kwenda Arsenal wakati wa dirisha dogo la usajili barani Ulaya kwa dau la £ 56 milioni takribani shilingi bilioni 117. Nyota huyo leo atakuwa anaiwakilsiha Arsenal kwenye fainali ya kombe la ligi EFL dhidi ya Manchester City.
-
Vurugu za mashabiki zasababisha kifo cha askari
-
Watatu Chelsea kuikosa Man Utd kesho
-
Mourinho adai anasubiri muda ufike achukue pointi tatu kwa Chelsea