Kiungo kutoka nchini Uganda Khalid Aucho amesema yupo tayari kuikabili AS Real Bamako katika mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kudi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans itakua mwenyeji wa mchezo huo, Jumatano (Machi 08) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikihitaji matokeo ya ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga Robo Fainali.

Aucho ambaye alipata majeraha katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi D, dhidi ya AS Real Bamako uliopigwa Jumapili (Februari 26) mjini Bamako-Mali.

Amesema anafahamu umuhimu wa mchezo huo, huku akiwashukuru madaktari wa timu hiyo kwa huduma ya kwanza aliyoipata uwanjani, kabla ya kurejea Tanzania.

“Ninaendelea vizuri hivi sasa baada ya kupatiwa huduma ya kwanza palepale uwanjani, kisha baada hapo matibabu yaliendelea.”

“Awali madaktari walidhani nimepata jeraha la goti lakini baada ya kunifanyia vipimo nikaonekana nipo vizuri isipokuwa nina michubuko tu chini ya goti.”

“Nipo tayari kucheza mchezo ujao dhidi ya AS Real Bamako watakapokuja hapa Dar es salaam kama kocha akinihitaji kunitumia, hivyo mashabiki wa Young Africans waondowe hofu.” amesema Aucho

Young Africans ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D ikiwa na alama nne, ikitanguliwa na US Monastir ya Tunisia yenye alama saba.

TP Mazembe ya DR Congo ipo nafasi ya tatu kwa kufikisha alama tatu, huku AS Real Bamako ya Mali ikiburuza mkia kwa kuwa na alama mbili.

Rais Young Africans atangaza vita Afrika
Rais Samia azuia mawaziri kuajiri maafisa habari binafsi