Msanii wa Nigeria,Wizkid anazidi kuyakuna masikio ya wasanii wakubwa wa kimataifa.Miezi michache baada ya kuisikia sauti ya Rihanna ikimwambia “you are amazing” alipokuwa akiimba booth huko Marekani, sasa msanii huyo amekuwa surprised na sauti ya Drake kwenye wimbo wake Ojuelegba.

Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi wala kuzungumziwa kabla na Wizkid, ilisambaa remix ya wimbo wa Wizkid ‘Ojuelegba’ ukiwa na sauti ya Drake ambaye amerap vizuri baada ya kusikika Skepta ambaye ni rapper mzawa wa Uingereza.
Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Wizkid ambaye ameweka wazi kupitia twitter jana asubuhi kuwa anatarajia kuachia nyimbo tatu alizofanya na mkali wa RnB, Chris Brown.

“We just getting Started! I got 3 songs with Chris Brown! We gonna f*** up the air waves! Respect the Sound! #Starboy”, alitweet.

Kwa harakati hizi na kukubalika huku kwa wasanii wakubwa wa Afrika katika masikio ya wasanii wa ‘A List’ ya Marekani, tunaamini kutawashtua BET wakome kutoa tuzo kwa wasanii hawa nyuma ya jukwaa la tuzo hizo.

Usikilize hapa:

January Makamba: Magufuli Atarejesha Imani Kwa CCM
Mila Kunis Aithibitisha Ndoa Na Ashton Kutcher Na Kumiliki Bunduki