Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yupo kwenye ziara katika wilaya za Dar es salaam akiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea ufafanuzi papo hapo, ambapo siku ya leo Novemba 25, 2016 amefanya ziara katika Wilaya ya Ubungo.

unnamed-1 rc-makonda-ubungo-2

Akiwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Maramba Mawili Makuti katika kata ya Mbezi, Makonda amekutana na kero ya wananchi wakilalamikia kubomolewa nyumba zao na wakala wa barabara TANROADS kwa lengo la upanuzi wa barabara licha ya kudai kushinda kesi.

Katika kutatua kero hiyo hatua za kutatua kero hiyo, imempelekea Makonda kuwasiliana na Rais Magufuli kwa njia ya simu na akalitolea ufafanuzi suala hilo na mambo mabalimbali kama inavyojieleza kwenye Audio hapo chini.

TPSF yaiomba Serikali kuboresha sera ya wajasiriamali
Makamba awataka wazanzibar kuulinda muungano