Aliyekuwa mgombea Urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa amesema Rais Magufuli anafanya kazi vizuri ikiwa ni pamoja na mambo yanayowagusa wananchi kama utendaji hafifu na juhudi za kupambana na ufisadi. Lowassa amesema kuwa pamoja na utendaji mzuri wa Rais Magufuli wao (UKAWA) wangekuwepo madarakani wangefanya vizuri zaidi kama suala la elimu ambapo yeye angeanza na mishahara ya walimu na si madawati.
Lowassa amesema hayo leo Deptemba 15, 2016 katika mahojiano na BBC Swahili, Nairobi Kenya ambapo amesema katia ya mambo yanayofanikisha CCM kuwa madarakani ni historia ya chama hicho na kuwepo vijijini zaidi kuliko vyama vingine vya upinzani. Lowassa pia ameelezea sakata la katiba mpya. Bofya hapa kusikiliza zaidi (Audio)