Tetemesha Entertainment ambayo iliwatambulisha na kuwainua wasanii kama Barakah Da Prince, Hussein Machozi na Sajna, imemtambulisha msanii mpya kutoka mwanza anayefahamika kama ‘Coyo’.

Msanii huyo ambaye aliiteka Kanda ya Ziwa kwa wimbo wake wa kwanza ‘Noma’, ameachia wimbo wake wa kwanza akiwa chini ya Tetemesha, alioupa jina la ‘Njoo Baadae’.

“Ninamzungumzia mtu anayekuchanganyia mafaili kwa stori (umbea) muda ambao unamishe zako ambazo haziendani na stori zake, hivyo unaamua kumchana habari hizo apeleke kwa zinaowahusu au aje baadae,” Coyo ameiambia Dar24 kuhusu ujumbe wa wimbo huo.

Ndani ya nyimbo zote mbili kuna mchanganyiko wa rap nzuri na baadhi ya maneno ya lugha ya kisukuma.

‘Njoo Baadae’ imeandaliwa na watayarishaji watatu, Mr T Touch, mtayarishaji mpya aitwaye Daydream pamoja na KidBway chini ya usimamizi wa Tetemesha Entertainment.

Usikilize hapa:

Makamba awataka wazanzibar kuulinda muungano
Makonda atoa agizo kwa meya wa ubungo