Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Lyatonga Mrema (77), amefariki.

Mrema amefariki hii leo Agost 21, 2022, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam alipokuwa amelwazwa tangu Agosti 16,2022.

Akithibitisha kifo hicho, Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema Mrema alilazwa hospitalini hapo na amefariki majira ya asubuhi hii leo Jumapili.

Augustino Lyatonga Mrema, (Desemba 31, 1944) – (Agosti 21, 2022).

Augustino Mrema, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini, ikiwemo Uwaziri wa Mambo ya Ndani na pia aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mrema pia aliwahi kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi mwaka 1995, baada ya kujiunga nacho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema pia amewahi kuwa Mbunge Vunjo kupitia Chama chake cha Tanzania Labour Party (TLP) na hadi umauti unamfika alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, nafasi ambayo aliteuliwa kwa mara ya kwanza Julai 16, 2016.

Mwili wa Dos Santos hatimaye wawasili Angola kwa maziko
Malipo ya Zuchu kujitoa WCB ni Bil. 10