Muigizaji wa filamu, Aunt Ezekiel ambaye alikuwa akiunga mkono kambi ya vyama vinavyounda Ukawa, amezua sintofahamu kwa wafuasi wa kambi hiyo baada ya kusambaa taarifa zinazodai amehamia CCM.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinazosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii zinadai kuwa muigizaji huyo ameihama kambi ya Ukawa baada ya kufanya mazungumzo ya siri na upande anaotakiwa kuhamia huku ikidaiwa kuwa alipewa fedha.

Aunt EZ UKAWA

Baada ya taarifa hizo kuenea, wafuasi wa chama hicho wamekuwa wakimuuliza kupitia posts zake za Instagram kuhusu ukweli wa jambo hilo lakini amekuwa kimya.

Hata hivyo, hali inaonesha kuwa huenda taarifa za kuihama kambi hiyo zikawa na ukweli kutokana na mwenendo wa hivi karibuni wa muigizaji huyo kupitia Instagram ambapo alikuwa akipost mara kwa mara picha za harakati za Ukawa na mgombea wao wa urais, Edward Lowassa.

Ingawa wafuasi wa Ukawa na CCM walikuwa na kiu ya kufahamu msimamo wake, Aunt Ezekiel alipost picha na kuonesha utani kuhusu msimamo wake wa siasa.

“Huyu ni Rk na hii ni Pizza jaman Sio CHADEMA Wala CCM Haya twende sasa… @lyabekim” aliandika.

Huyu ni Rk na hii ni Pizza jaman Sio CHADEMA Wala CCM Haya twende sasa….. ? @lyabekim

A photo posted by Auntyezekiel??? (@auntyezekiel) on

Presha inayotokana na taarifa hizo zisizo na majibu ya moja kwa moja kutoka kwa mhusika imepelekea mashabiki wa Ukawa kumshambulia huku wengine wakipinga mashambulizi hayo kutokana mkanganyiko uliopo.

 

Zitto Kabwe Awapigania Slaa Na Lipumba, Akosoa Ahadi Ya Magufuli
Maandishi Ya Mkono Ya Tupac Akiwa Jela Kuuzwa Mamilioni