Ni kawaida kwa Australia kupata majanga ya moto katika kipindi ambacho kinafahamika kwa jina la Fire Season (Msimu wa Moto), ila kwa sasa inakabiliwa na hali ngumu zaidi ambayo inasababishwa na kupanda kwa joto na miezi ya ukame uliokithiri.
Hii inadaiwa kuwa ni tukio kubwa la moto kuwahi kutokea nchini humo ambapo mpaka sasa moto huo umezalisha zaidi ya tani 250 za Hewa ya ‘Carbondioxide’.
Imeelezwa kuwa moto huo wa nyika unaoendelea kusambazwa na upepo, umeua watu 20, wanyama 500 na kuteketeza ekari milioni 15 pamoja na makazi ya watu.
Japo moto ni kitu cha kawaida kwa hali ya hewa ya Australia, lakini wanasayansi walitahadharisha kuwa kipindi hiki moto utakuwa mkali zaidi ya ilivyozoeleka na utabiri unaonesha moto huo unaweza kuendelea kuwaka kwa wiki moja zaidi.