Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema Julian Assange yuko huru kurejea nyumbani baada ya kutatua matatizo yake ya kisheria.

Morrison ameyasema hayo leo baada ya mahakama ya Uingereza jana kupinga ombi la kutaka muasisi huyo wa shirika la kimataifa la ufichuzi WikiLeaks ahamishiwe Marekani.

Morrison amesema mfumo wa sheria unafanya kazi yake na kuwa nchi haiwezi kuingilia kwa sasa lakini Assange, kama raia mwingine yeyote wa Australia, ana haki ya kupewa msaada ubalozini na kuwa baada ya kesi yake, yuko huru kurejea nyumbani.

Assange, mwenye umri wa miaka 49, alishitakiwa Marekani kwa makosa 18 wakati wa utawala wa Rais wa zamani Barack Obama yanayohusiana na uvujishaji uliofanywa na tovuti ya WikiLeaks wa nyaraka za siri za jeshi la Marekani na za kidiplomasia ambazo wanasema ziliyaweka maisha ya watu hatarini.

Dkt. Mwinyi na Maalim Seif wafungua jengo la ZSSF
Kilo 4,880 za Sukari ya magendo zagawanywa kwenye taasisi

Comments

comments