Mzee mmoja aliyetambulia kwa jina la Tuntinala Kunyepa (75) mkazi wa Kijiji cha Ihanda Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, amekutwa ameuawa na kuchunwa ngozi na kisha kutolewa baadhi ya viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, Yusuph Sarungi, amesema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hiilo huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina ambapo uchunguzi na msako mkali unaendelea kuwabaini waliohusika.
Hata hivyo, mauaji kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara ambapo yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina.