Wachezaji Kennedy Musonda wa Klabu ya Young Africans na Clatous Chama wa Simba SC, wametajwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Zambia, kitakachoikabili Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.
Wachezaji hao wametajwa katika kikosi cha Chipolopolo, kufuatia uwezo wanaoendelea kuuonesha wakiwa na Klabu zao za Tanzania katika Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa msimu huu 2022/23.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zambia Avram Grant alifika Tanzania kufuatilia mchezo wa Simba SC dhidi ya Vipers SC (Uganda), kisha alifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Young Africans na AS Real Bamako (Mali), na huenda alilidhishwa na uwezo wa wachezaji hao.
Hata hivyo Mshambuliaji wa Simba SC Moses Phiri ameachwa katika kikosi cha Zambia, huku majina ya washambulaiji wengine yakionekana katika orodha ya kikosi kilichoanikwa hadharani leo Ijumaa (Machi 17).
Wachezaji wanaocheza nafasi ya Ushambuliaji walioitwa katika kikosi cha Zambia ni Joseph Phiri (Red Arrows), Lazarus Kambole (ZESCO United), Lameck Banda (US Lecce – Italy), Fashion Sakala Jnr (FC Rangers – Scotland), Patson Daka (Leicester City – England), Kennedy Musonda (Yanga SC – Tanzania) na Edward Chilufya (Midjtlland – Denmark).
Wengine walioitwa kuunda kikosi cha Chipolopolo upande wa Walinda Lango ni Allan Chibwe (Forest Rangers), Lawrence Mulenga (Power Dynamos), Toaster Nsabata (Sekhukhune United).
MABEKI: Benedict Chepeshi (Red Arrows), Dominic Chanda (Kabwe Warriors), Teddy Kumalo (Atletico Lusaka), Aaron Katebe (Power Dynamos), Rodrick Kabwe (Sekhukhune United), Frankie Chisenga Musonda (AYR – Scotland), Tandi Mwape (TP Mazembe) na Aime Mabika (Inter-Miami, USA)
VIUNGO: Kelvin Kapumbu, Kelvin Kampamba (both Zesco United), Patson Kwataime (Mighty Mufulira Wanderers), Emmanuel Banda (HNK Rijeka – Croatia), Klings Kangwa (Crvena Zvezda – Serbia), Lubambo Musonda (AC Horsens – Denmark), Benson Sakala (Pribram – Czech Republic), Clatous Chota Chama (Simba SC – Tanzania) na Rally Bwalya (Amazulu – South Africa).