Mwimbaji wa kike toka Kenya, Avril amezungumzia taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa anaujauzito kutokana na picha za nguo za mtoto alizopost kwenye Instagram zilizoambatana na maelezo yaliyoashiria ujio au uwepo wa kichanga.

Ingawa marafiki zake wa karibu walijitokeza kumpongeza kupitia mtandao huo na yeye kuonesha kila dalili za kuzipokea, mkali huyo wa ‘Kitu Kimoja’ amekanusha kuwa mjamzito alipoongea na kipindi cha Mambo Mseto.

Avril ameeleza kuwa nguo na viatu alivyopost ni vya mtoto wa kiume wa mdogo wake, hivyo alikuwa na furaha ya kuwa shangazi na sio mama kama wengi walivyotafsiri.

Ndugu wa Kim Kardashian apozi mtupu kuuza bidhaa za ‘Calvin Klein’
R. Kelly Ashitakiwa Na Kaka Yake Wa Damu Kwa Dhuruma