Naibu waziri wa maji, Jumaa Aweso ameagiza mhandisi wa manispaa ya Temeke, Damas Shirima kukamatwa na kuhojiwa na polisi kwa kosa la kutoa maelezo yasiyo ridhisha juu ya utekelezaji wa mradi wa maji wa mwasongo uliopo Kigamboni Dar es salaam.
Akizungumza katika majumuisho ya siku yake ya pili ya ziara yake jijini Dar es salaam, Aweso amesema kuwa serikali haiwezi kunyamaza kimya pale inapoonekana miradi ya maji inahujumiwa na kwamba watahakikisha wale wote ambao wanagundulika kuhujumu miradi ya maji hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo, mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa jimbo lake bado linachangamoto ya upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo ambapo ameahidi kulisimamia suala hilo ili wananchi waondokane na kero hiyo.
-
Shonza awataka waandishi wa habari kuzingatia maadili
-
Dkt. Mwakyembe ayafunda mashirikisho ya Sanaa na Filamu
-
Serikali yabaini njia zinazotumiwa kupitisha dawa za kulevya