Waziri wa Maji,  Jumaa Aweso amemkurugenzi mtendaji wa maji safi na usafi wa mazingira wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Robert Lupoja kisha kumteua Sadala Hamis kushika nafasi hiyo.

 Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo leo Jumatatu Juni 14, 2021 imeeleza kuwa uteuzi wa Hamis unaanza mara moja.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa katika hatua nyingine, Aweso ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sengerema huku taratibu nyingine zikiendelea kufanyiwa kazi.

Mgonjwa anayehitaji damu ahudumiwe kwanza huku taratibu zingine zikifuatwa – Dkt. Mollel
RC Kunenge aagiza uchuguzi kwa watumishi Mkoa wa Pwani