Waziri wa Maji Jumaa Aweso amekagua mtambo mkubwa wa kuchuja maji chumvi katika eneo la Serengeti, Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro ili kujiridhisha na huduma ya majisafi inayotolewa kwa wananchi.
Waziri Aweso amefanya ziara hiyo ya kikazi lengo kuu likiwa kuboresha hali ya upatikanaji wa Majisafi na salama wilayani Gairo.
Aidha amewataka watalaamu kufanya kazi ya utafiti na kuchimba visima virefu eneo la Ngiloli ili kuongeza haraka iwezekanavyo kiasi cha majisafi kwa wananchi mjini Gairo.
Sambamba na hayo Waziri Aweso ameagiza tathmini na hatua za awali zifanyike ili kuweza kutoa maji kutoka chanzo cha maji cha Chagongwe kupeleka mjini Gairo ikiwa ni mpango wa kudumu utakaomaliza changamoto ya uhaba wa huduma ya majisafi.
Pia amewataka EWURA kufanya kazi ya tathmini ya bei ya majisafi inayotumika mjini Gairo endapo inaendana na uhalisia wa gharama za uendeshaji ili wananchi wasiumie katika kupata huduma ya majisafi.