Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ametangaza kiama kwa watakaobainika kula fedha za mradi wa maji kijiji cha Ukarawa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe na kwamba watazitapika.

Ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya siku nne Mkoani Njombe ambapo akiwa wilayani Njombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ukarawa mara baada ya kukagua mradi wa maji ambao serikali imeshamlipa mkandarasi milioni 530 katika mradi huo.

‘’Mradi huu ni wa miaka mingi wakati mwengine mnasababisha mama zetu wanashindwa kupaka mafuta wala poda kutokana na kukosekana kwa maji’’amesema Aweso.

Aidha, mhandisi wa maji wa halmashauri ya wilaya ya Njombe, Rajab Yahaya amemueleza naibu waziri juu ya matumizi ya fedha ambapo milioni 10 hazijulikani zilipo.

Hata hivyo, Naibu waziri huyo amesema kuwa lazime ifike hatua watu waogope fedha kutafuna fedha za miradi ya maji.

 

Video: Kauli ya Bashiru yagonga vichwa, Waliokusanya kodi 'kiduchu' matatani
Waziri Kamwelwe awatimua Wachina wawili nchini