Waziri Wa Maji, Jumaa Aweso amefanya ziara katika Mkoa wa Manyara ambapo ametembelea jimbo la Babati Vijijini kukagua miradi mbalimbali ya maji

Waziri Aweso amekagua mradi mkubwa wa maji Minjingu na kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao umefika asilimia 95 na ametoa maelekezo mradi huo uwe umekabidhiwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2021.

Pia Waziri Aweso amekagua mradi wa maji Darakuta, Magugu ambayo umefikia asilimia 75 Waziri amerizishwa na mwenendo wa mradi huo na kuwaagiza wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili wananchi waaanze kupata huduma

Katika ziara hiyo Waziri Aweso ameongozana na Mbunge wa Jimbo hilo Daniel Sillo, Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange ambapo wamezindua mradi wa maji uliokamilika wa Endakiso ambao umeanza kufanya kazi.

Shikalo kurudi Kenya
Wagombea hawakuwa wakikubalika - Mbowe