Kwa lugha ya kigeni iliyobeba muktadha wa utamaduni wa hip hop tunasema ‘real recognize real’, kwa tafsiri ya kijumla ni ‘wakali hujuana na kuheshimiana’. Hivyo ndivyo AY alivyofanya kwa Joh Makini.
AY ameeleza kuwa katika kipindi chote cha miaka 9 iliyopita, kati ya wasanii waliojitosa kwenye game ya rap ndani ya kipini hicho hakuna hata mmoja anayeweza kuufikia uwezo wa mweusi Joh Makini.
“Hakuna rapa mwingine aliyeingia kwenye ‘game’ baada ya mwaka 2008 akawa mkali kumzidi Joh Makini,” AY ameiambia Planet Bongo.
Joh Makini na AY wameachia ngoma zao mpya hivi karibuni wakipishana siku chache. AY akiwa na Nyashinski kutoka Kenya ameshusha mzigo wa ‘More & More’. Mweusi toka Arusha ameleta gumzo mtaani na ‘Waya’ iliyoambatana na video.
Ingawa Joh Makini alianza muziki kitambo akiwa Arusha, tangu alipokuwa akijiita ‘Rapture’, aliingia kwenye rap ya ushindani na biashara rasmi mwaka 2006 na kuanza kuiteka mitaa na ngoma zake kali mfululizo zikiwemo ‘Hao, Chochote Popote na nyingine’ akiwa jijini Dar es Salaam. Hivi sasa amevuka mipaka na amefanya collabo na wasanii wakubwa Afrika akiwemo AKA wa Afrika Kusini.