Mwanamuziki nguli wa hip hop Tanzania Ambwene Yesaya maarufu AY, ametangaza rasmi ujio wa wimbo wake mpya akishirikiana na muimbaji nyota wa kundi la Sauti Sol kutoka nchini Kenya Bien Sol.
AY amedokeza ujio huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kama sehemu ya kuwaandaa mashabiki wake juu ya wimbo huo mpya ambao bado jina lake halijawekwa wazi.
Hi ni mara ya kwanza kwa AY kushirikiana na Bien Soul kama solo artist lakini ikumbukwe zaidi ya miaka tisa iliyopita rapa huyo alilishirikisha kundi zima la sauti sol ambalo ndani yake alikuwamo Bien na wenzie watatu kwenye wimbo uliofanya vizuri sana wakati huo ‘I don’t wanna be alone.’
Wimbo huo mpaka leo Sauti Sol huuzungumzia wakimshukuru rapa AY kwa kuwashirikisha na kwamba ndio ulikuwa wimbo uliochagiza safari yao kimuziki kuwa yenye mafanikio zaidi kutokana na kupata wafuasi wengi punde baada ya kolabo hiyo.