Lugha ya kiswahili sasa, inaendelea kuenea kwa kasi sehemu kubwa ya bara la Afrika hata kufikia hatua ya kuanza kutumika na wasanii wa muziki kutoka mataifa yasiyozungumza lugha hiyo akiwamo mwimbaji Ayanfe kutoka nchini Nigeria ambaye kupitia wimbo wake ‘Laba Laba’ ametumia maneno ya kiswahili akichanganya na baadhi ya maneno ya ki-Yoruba, wimbo wenye mahadhi ya Amapiano aliomshirikisha Dj Latitude pamoja na Lam Beatz.

Nyota huyo anayeonyesha kiu ya kuhitaji kuiteka Afrika mashariki, hivi karibuni ameweka wazi kuwa anatarajia kufanya ziara yake ya kimuiziki, katika mataifa ya Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, Kenya na Uganda kama sehemu ya kujisogeza karibu na sehemu kubwa ya mashabiki wa muziki wake.

Ayanfe ambaye hivi karibuni alisaini mkataba wa kurekodi na Alpha Nation anatarajiwa pia kutoa Extended playlist yake, ambayo amebainisha kuwa tayari imekamilika na wasanii wakubwa kutoka Nigeria hasa kutoka lebo ya DMW inayomilikiwa na mwanamuziki Davido,.

Pamoja na hayo ikumbukwe kuwa miaka miwili iliyopita. nyota huyo alifanya kazi na Mayorkun iitwayo ‘Whats goin on’ na mwaka 2022 akaachia wimbo alioshirikiana na Davido iitwayo ‘Migrate’.

Kufuatia ziara yake hiyo ikiambatana na mkakati wa kuachia EP yake, mashabiki wa Ayanfe wamefahamishwa kukaa mkao wa kula na kuwa tayari kupokea nyimbo zililizowakutanisha wasanii mbali mbali wa Afrika mashari.

CCM kuendeleza utekelezaji sera ya Afya, elimu bure
KMC FC yatamba kuisasambua Mbeya City
Tags