Kikosi cha Azam FC mapema leo asubuhi kilifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Amaan kabla ya kucheza na timu ya Kombaini ya Zanzibar, mchezo utakaopigwa kesho Jumatano saa 2.15 usiku.

Azam FC imeweka kambi kisiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoendelea mapema mwezi ujao, baada ya kumalizika kwa Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’.

Tayari Azam FC imeshacheza michezo miwili ya kirafii visiwani humo, dhidi ya Malindi FC waliokubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri, kisha KMKM walioibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Mchezo wa kesho dhidi ya Kombaini ya Zanzibar utakuwa wa mwisho wa kirafiki kwa Azam FC kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Ijumaa hii.

Azam FC iliweka kambi visiwani humo baada ya kutolewa kwenye Kombe la Mapinduzi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya mabingwa wa michuano hiyo Young Africans.

Matola: Morrison haumwi ‘MSHIPA WA NGIRI’
Pawasa auanika hadharani udhaifu wa Kisinda

Comments

comments