Klabu ya Azam FC imethibitisha taarifa za kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa Mara Tano wa Afrika TP Mazembe, kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza Mshike Mshike wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika 2022/23.

Azam FC itaanza kuonyesha makali yake katika Mzunguuko wa Kwanza wa Michuano hiyo kwa kukipiga dhidi ya Al-Akhdar Sports Club ya Libya, ikianzia ugenini kati ya Oktoba 7-9, na itamalizia nyumbani Azam Complex-Chamani kati ya Oktoba 14-16.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema mchezo huo wa Kimataifa wa Kirafiki umepngwa kuchezwa katika mji wa Ndola-Zambia, ambako TP Mazembe imeweka Kambi katika kipindi hiki cha kupisha michezo ya Kalenda ya ‘FIFA’.

Amesema TP Mazembe nao watautumia mchezo dhidi ya Azam FC kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC.

“Mchezo huu utakuwa wa kawaida ambao kocha wetu atautumia kuangalia wachezaji kwa lengo la kuhakikisha tunapata kikosi bora kabla ya kuivaa Al-Akhdar Sports Club ya Libya mapema mwezi Oktoba, kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho” amesema Zaka Zakazi

Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa, kikosi chao kitaondoka Dar es slaam keshokutwa Alkhami (Septemba 22) kuelekea mjini Ndola-Zambia, baada ya kupata Mwaliko wa TP Mazembe.

Amesisitiza kuwa, wanajivunia kupata mwaliko huo kutokana na TP Mazembe ni Klabu kubwa Barani Afrika na tayari wameshafanikiwa kutwaa Ubingwa wa Afrika mara tano, hivyo ni jambo sahihi kwao kucheza mchezo huo wa Kirafiki kwa maandalizi ya kujiweka sawa Kimataifa.

Hassan Mwakinyo: Watanzania punguzeni mihemko
Taifa Stars yazifuata Libya, Uganda