Mabingwa wa Afrika mashariki na kati *Kombe La Kagame* Azam FC, jana usiku ilimaliza ziara yake ya kambi maalum huko kisiwani Unguja kwa kuichapa timu ya JKU kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Amaan.

Azam ambayo ilipiga kambi maalum kisiwani humo kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya timu ya Yanga ilionyesha kandanda safi na kuvutia.

Alikuwa ni nahodha John Bocco ndiye aliyeanza kutingisha nyavu za JKU mnamo dakika ya 65 kwa bao safi na la kiufundi.

Kiungo Azam Abubakar Salum ndiye aliyeipatia azam bao la pili mnamo dakika ya 87 na mchezo kuisha kwa azam kutoka uwanjani kifua mbele kwa mabao 2-0.

Mabingwa hao wanatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam hii leo tayari kwa mchezo wa kuwani ngao ya jamii utakaochezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa taifa.

Mara baada ya kuwasili jijini humo Azam  FC watakwenda moja kwa moja kambini Chamazi Complex.

FC Barcelona Si Lolote Kwa Athletic-Bilbao
Ramos Akinzana Na Vyombo Vya Habari