Timu ya Azam FC baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho sasa nguvu zao watazielekeza kwenye ligi kuu soka Tanzania bara ambapo ratiba yao kwa mwezi Octoba itakua ni kucheza mchezo mmoja baada ya mwengine.

Kwa mujibu wa ratiba Azam fc watashuka dimbani kesho ambapo watakuwa na kibarua katika uwanja wa Azam Complex, kabla ya kumaliza na Simba mwishoni mwa mwezi ikiwa punde tu wametoka kutolewa ndani ya Ligi ya mabingwa Afrika na UD do Songo.

Hizi hapa mechi zake nne ambazo itacheza kwenye ligi na Azam FC, Ndanda, Octoba 2 uwanja wa Azam Complex.

Azam FC vs Namungo, Octoba 5, uwanja wa Azam Complex.

Azam FC vs JKT Tanzania, Octoba 19 uwanja wa Azam Complex.

Simba vs Azam FC, Octoba 23, uwanja wa Uhuru.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 2, 2019
TAKUKURU yataja ofisi za Serikali zenye kashfa ya Rushwa